Marekani hatimaye yatoka katika makubaliano ya Nyuklia na Iran

Marekani hatimaye yatoka katika makubaliano ya Nyuklia na Iran

Rais wa Marekani atangaza Rasmi kutoka katika makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran, huku akisisitiza kuwa ataongeza vikwazo vikali dhidi ya Iran

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Rais wa Marekani ametangaza rasmi kujitoa kwake katika makubaliano ya mapango wa Nyuklia wa Iran uliofanyika kati kikundi cha 5+1 na Iran, makubaliano ambayo yalifanywa mwaka 2015.
Aidha mwanzo wa mazungumzo yake amedai kuwa: Iran ni katika mataifa yanayounga mkono vikundi vya kigaidi ambapo vikundi kama Alkaida, Taleban, Hamasi na Hizbullah, akisisitiza kuwa Iran daima hutumia vibaya mali za taifa lake kuwapa silaha wapalestina na vikundi vingine vya kigaidi.
Aidha alikitoa madai kuwa Iran haikutekeleza masharti ya makubaliano hayo, ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Israel ni kwamba Iran inaendelea na harakati zake za kuizfikia silaha za Nyuklia na makombola ya Ballistic, hivyo kama niliposema hapo awali kuwa kama itashindikana kurekebisha makubaliano hayo, nitatoka katika mkataba hupo, hivyo nimeamua kujitoa katika makubaliano ya mpango wa Nyuklia kati ya Iran na 5+1.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky