Marekani kuiwekea vikwazo Urusi kwa kutumia silaha ya Sumu

Marekani kuiwekea vikwazo Urusi kwa kutumia silaha ya Sumu

Marekani imetangaza kuwa itaiwekea Urusi vikwazo, kufuatia jaribio lake la kutumia sumu inayoathiri mishipa kutaka kumuua jasusi wa zamani wa Urusi na bintiye nchini Uingereza.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Marekani imetangaza kuwa itaiwekea Urusi vikwazo, kufuatia jaribio lake la kutumia sumu inayoathiri mishipa kutaka kumuua jasusi wa zamani wa Urusi na bintiye nchini Uingereza. Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani, imesema hapo jana kuwa, imebaini kuwa Urusi ilitumia silaha ambayo imepigwa marufuku chini ya sheria inayopinga matumizi ya silaha za kemikali na kibaolojia. Kutokana na hatua hiyo ya kukiuka sheria ya kimataifa, Marekani itaiwekea vikwazo. Jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na bintiye walishambuliwa kwa sumu ya Novichok mwezi Machi mwaka huu, wakiwa katika mji wa Salisbury Uingereza. Uingereza iliilaumu Urusi kwa kuhusika na shambulizi hilo, lakini Urusi imekana.

Mwisho wa habari / 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky