Marekani, Uingereza, Ufaransa washambulia Syria

Marekani, Uingereza, Ufaransa washambulia Syria

Marekani ikishirikiana na Ufaransa na Uingereza wamefanya mashambulio ya anga katika mji mkuu wa Syria Dumascus

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Rais wa Marekani asubuhi ya leo ametoa tamko kuwa tumeshatoa amri rasmi ya kuishambulia Syria, akisisitiza hilo amesema kuwa asubuhi ya leo nimetoa amri ya kushambulia Syria, ambapo mashambulio hayo yanafanywa katika kambi za majeshi ya Syria ambazo zina mabomu ya kemikali.
Aidha ameongeza kusema kuwa: mashambuli hayo yameambatana na mashambulio ya majeshi ya Ufaransa na Uingereza, ambapo kwa upande wangu nayashukuru mataifa hayo kwa ushirikiano wao, na tutabainisha sababu ziliopelekea kuchukua maamuzi ya kuishambulia Syria.
Vyombo vya habari vya Syria vimetanga kusikika kwa sauti ya miripuko mizito ya mabomu, ambapo vyanzo muhimu nchini Syria vimesema kuwa baadhi ya mabomu, hayakuweza kuripua sehemu husika badala yake yaliripuka angani baada ya kukabiliana na vitengua mapumu vya majeshi ya Syria.
Baadhi ya vyombo vya habari vya mataifa ya kiarabu yametangaza kuwa: makombora 100 yalishambulia maeneo mbalimbali nchini Syria ambayo yalipigwa na majeshi ya Marekani,   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
We are All Zakzaky