Marekani yaiasa Korea Kaskazini kusimamisha mipango yake ya makombora ya nyuklia

Marekani yaiasa Korea Kaskazini kusimamisha mipango yake ya makombora ya nyuklia

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ameitaka Korea Kaskazini kuachana na mipango yake ya kutengeneza makombora na silaha za nyukilia na kusema kuwa taifa hilo lililotengwa haliwezi kuitisha Marekani.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ameitaka Korea Kaskazini kuachana na mipango yake ya kutengeneza makombora na silaha za nyukilia na kusema kuwa taifa hilo lililotengwa haliwezi kuitisha Marekani. Tillerson ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na Waziri wa mambo ya nje wa Japan Fumio Kishida mjini Tokyo ambako walijadili njia mpya ya kushughulikia suala hilo la Korea Kaskazini. Amesema juhudi za kidiplomasia pamoja na njia nyingine zilizofanyika katika kipindi cha miaka 20 za kuishawishi Korea Kaskazini kuachana na mipango yake hiyo zimeshindwa. Hata hivyo waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani hakuelezea ni jinsi gani utawala wa Rais Donald Trump ambao hivi sasa unapitia upya sera za nchi hiyo utakavyoshughulikia suala hilo. Amefafanua kuwa mpango huo wa Korea Kaskazini ni wa hatari na ni kinyume cha sheria. Korea Kaskazini kwa muda mrefu imekuwa ikitaka kufikia makubaliano ya amani na Marekani yakilenga kuchukua nafasi ya mkataba uliokomesha vita vya Korea katika kipindi cha kati ya mwaka 1950 hadi 1953. Hii ni ziara ya kwanza ya Tillerson barani Asia tangu ashike wadhifa huo wa waziri wa mambo ya ne wa Marekani.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky