Marekani yaituhumu tena Syria kwa mashambulizi ya Sumu

Marekani yaituhumu tena Syria kwa mashambulizi ya Sumu

Marekani imetangaza kuwa raia kadhaa wa Syria wanatibiwa baada ya kushindwa kupumua kutokana na mashambulizi sumu ya ndege yaliyofanywa na serikali kwenye mji wa Saraqeb.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Marekani imetangaza kuwa raia kadhaa wa Syria wanatibiwa baada ya kushindwa kupumua kutokana na mashambulizi sumu ya ndege yaliyofanywa na serikali kwenye mji wa Saraqeb.

Shirika linalofuatilia haki za binaadamu nchini Syria lenye makao yake mjini London, Uingereza limesema raia watano wanapatiwa matibabu kutokana na kukosa pumzi na kushindwa kupumua baada ya kile walichodai kuwa serikali ya Syria kutumia silaha za sumu katika maeneo yanayodhibitiwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani kwenye mji wa Saraqeb uliopo kaskazini magharibi mwa Syria.

Shambulizi hilo linadaiwa  kufanyika siku chache baada ya Marekani kuishutumu serikali ya Syria kwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya vikosi vya magaidi karibu na mji mkuu, Damascus.

Hata hivyo serikali ya Syria imekanusha vikali madai hayo ikiyaita kuwa ni ''uongo''. Siku ya Ijumaa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Jim Mattis aliwaambia waandishi habari kwamba serikali yake ina wasiwasi gesi ya sarin huenda ikawa imetumika hivi karibuni nchini Syria, ikizinukuu taarifa za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na makundi ya magaidi.

Marekani haina ushahidi juu ya madai yake

Hata hivyo, Mattis alisema hana ushahidi kuhusu madai hayo. Mwezi uliopita watu 21 walitibiwa kutokana na matatizo ya kupumua baada ya roketi kurushwa katika ngome ya waasi Mashariki mwa Ghouta, nje kidogo ya Damascus.

Shirika hilo limesema raia wengine 10 wameuawa katika jimbo la Idlib baada ya helikopta kushambulia maeneo kadhaa, huku watu watano wakiwa na matatizo ya kupumua, kutokana na taarifa kwamba gesi ya sumu ilitumika. Raia wengine wanne wameuawa na majeshi ya serikali katika maeneo ya Maaret al Numan na Maasarin.

Mkurugenzi wa vikosi vya ulinzi wa raia, Abu Hamdo amedai kuwa ndege zinazoaminika kuwa za Urusi zilishambulia hospitali ya Maaret al Numan na kusababisha uharibifu mkubwa.

''Ndege zimeanzisha mashambulizi makali na kuharibu jengo la ghorofa saba na jingine la ghorofa nne. Tumepata jumla ya miili sita na mtoto mmoja amejeruhiwa,'' alisema Hamdo.

Hata hivyo weledi wanalauu Marekani na Magaidi kwa wakitumia vyombo vya habari kutangaza taarifa za uzushi ili kushinikiza mataifa dhidi ya serikali ya Syria.

Mwisho wa habari / 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky