Marekani yakiri kuuwa raia wasiokuwa ba hatia 900 nchini Iraq na Syria

Marekani yakiri kuuwa raia wasiokuwa ba hatia 900 nchini Iraq na Syria

Umoja wa kupambana na ugaidi nchini Iraq na Syria chini ya usimamizi wa serikali ya Marekani, umekiri kuhusika na mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia takriban 900 kufuatia mashambulizi ya anga yanayofanywa na umoja huo nchini Syria na Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kiongozi mkuu wa umoja huo wa kimataifa dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh ameeleza hayo katika ripoti yake ya mwezi na kusisitiza kuwa toka mwaka mwezi Agosti mwaka 2014 mpaka sasa takriban kwa ujumla mashambulizi ya anga 2935 yamefanywa katika ardhi za Iraq na Syria.
Aidha akiendelea kusema hayo alibainisha kuwa kwa wa ripoti tulionayo kwa uchache wananchi wa kawaida 892 wamepoteza maisha kufuatia mashambulizi hayo, alkadhalika katika ripoti aliokuwa ametoa hapo kabla ambapo ilikuwa ni ya mwezi wa nne alitangaza kuwa wananchi waliouwawa ambao hawakuwa na hatia nchini Iraq na Syria alithibitisha kuwa ni watu 83.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky