Marekani yataka Umoja wa Mataifa kuchukua kuishitaki Iran

Marekani yataka Umoja wa Mataifa kuchukua kuishitaki Iran

Marekani imekuwa ikisaidia silaha nzito utawala wa saudia arabia na washirika wake, silaha ambazo zinatumika dhidi ya wananchi wasio na uwezo wa Yemen kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema ni wakati kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kufuatia kuchapishwa kwa ripoti na wataalamu wa Umoja huo inayoonyesha kwamba Iran ilikiuka vikwazo vya silaha nchini Yemen. Ripoti hiyo imeonyesha kwamba Iran ilishindwa kuzuia usambazaji wa silaha za makombora kwa wapiganaji wa Houthi walioko Yemen, ambayo yalifyatuliwa kuelekea Saudia Arabia. Haley alinukuliwa akisema "dunia haitaendelea kuvumilia ukiukwaji huu wa wazi kutopatiwa majibu na kwa maana hiyo Iran italazimika kujutia vitendo vyake. Iran yenyewe imekanusha vikali kuwapa silaha wapiganaji wa Houthi na kumtuhumu Haley kwa kuwasilisha ushahidi wa "kutunga" kwamba kombora lilifyatuliwa Novemba 4 kuelekea uwanja wa ndege wa Riyadh lilitengenezwa nchini Iran. Wanadiplomasia wanasema ukiukwaji huo wa Iran unatarajiwa kujadiliwa katika muswada wa maazimio ya kuangaziwa upya kwa vikwazo ambao baraza hilo linajiandaa kuupitisha baadae mwezi huu.

Marekani imekuwa ikisaidia silaha nzito utawala wa saudia arabia na washirika wake, silaha ambazo zinatumika dhidi ya wananchi wasio na uwezo wa Yemen kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Mwisho wa habari / 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky