Marekani yataka vita kusitishwa Yemen

Marekani yataka vita kusitishwa Yemen

serikali ya Marekani ambayo ni msaidizi mkuu wa Saudia arabia imetaka kusitishwa mapigano nchini Yemen na kufanyika mazungumzo ya amani huku muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen.

Shirika la habari la ABNA linaripti kuwa: serikali ya Marekani ambayo ni msaidizi mkuu wa Saudia arabia imetaka kusitishwa mapigano nchini Yemen na kufanyika mazungumzo ya amani huku muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis ametaka kuwepo makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Yemen na pande zinazozana kufanya mazungumzo katika kipindi cha siku thelathini zijazo.

Mattis amesema Marekani imekuwa ikiutizama mzozo wa Yemen kwa muda wa kutosha na anaamini Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu ambao ni washirika muhimu wa muungano wa kijeshi unaoungwa mkono na Marekani dhidi ya wananchi wa Yemenwako tayari kwa mazungumzo.

Waziri huyo wa ulinzi wa Marekani amesema muda umewadia wa kufanya mazungumzo ya kutafuta amani na kuzitaka pande zinazozana kukutana na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen Martin Griffiths nchini Sweden mwezi ujao ili kufikia suluhisho.

Je, mapigano yatatulia Yemen?

Naye waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ametaka mashambulizi yote ya angani yanayofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia kusitishwa mara moja katika maeneo yaliyo na makazi ya raia.

Aidha amewataka wapiganaji wa Houthi kukoma kurusha makombora na kufanya mashambulizi kwa kutumia ndege zisizoendeshwa na marubani dhidi ya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Zaidi ya watu 10,000 wameuawa katika mzozo huo wa Yemen na zaidi ya watu milioni 22 ambayo ni theluthi mbili ya idadi jumla ya Wayemeni wakihitaji misaada ya kibinadamu na wengine milioni 8.4 wako katika hatari ya kufa njaa.

Yemen ni moja ya mataifa masikini zaidi ya kiarabu na limekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka minne iliyopita.

Mahusiano kati ya Marekani na Saudi Arabia yamepooza katika wiki za hivi karibuni

Marekani imekuwa ikishutumiwa vikali kwa kuunga mkono muungano huo wa kijeshi unaoongozwa na Saudia hasa baada ya mashambulizi kadhaa ya angani kuwalenga raia kwa makusudi.

Mwisho wa habari / 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky