Mashambulizi ya kuikomboa Tal Afar yatangazwa kuanza/ Al-Abadi: magaidi Ima wajisalimishe au waangamie

Mashambulizi ya kuikomboa Tal Afar yatangazwa kuanza/ Al-Abadi: magaidi Ima wajisalimishe au waangamie

Mashambulizi ya kuikmboa Tal Afar nchini Iraq yaanza kwa amri ya waziri mkuu wa nchini hiyo, ambapo mji wa Tal Afar ni moja kati ya miji ambayo asilimia kubwa ya wakazi wake ni wafuasi ya madhehebu ya Shia, ambapo kikundi cha kigaidi cha Daesh kiliuteka mji huo toka miaka miwili iliopita

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA:waziri mkuu wa Iraq ambaye pia ni kamanda mkuu wa majeshi ya Iraq ametangaza rasmi kuanza kwa mashambulizi ya kuukomboa mji wa Tal Afar nchini humo.
Aidha waziri huyo amesema: wananchi wa Iraq ni wananchi watukufu wenye uchungu na taifa lao, ambapo kwa uwezo wa mwenyezi Mungu wananchi wetu tunawapa ahadi nyingine ambayo tunamuomba Mungu atukubalie ambayo ni kuuukomboa mji wa Tal Afar kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Al Abadi amesisitiza kuwa: tunawaambia magaidi wote wa Daesh kuwahawana njia yeyote kinyume na njia hizi kwamba ima wajisalimishe au wakubali kuangamia.
Kama tulivyowaahidi hapo mwanzo, hivi sasa pia tunarudia kuwaahidi kuwa tutaenedelea kuyakomboa maeneo yote ya Iraq, pia magaidi wa Daesh wanapaswea kuwa sehemu zote tuliopambana nao bilashaka tuliwashinda na kuwasambaratisha, hivyo wanapaswa kujifunza na kuwa na mazingatio katika jambo hili, ambapo vikundi vya kigaidi katika sehemu zote walishindwa na kuangamia!
Al-Abadi aliendelea kusema kuwa: natumia nafasi hii kuwatolea salamu za dhati kwa vikosi vyote ambavyo vimejiandaa ipasavyo katika mapambano haya ya kuukomboa mji wa Tal Afar, huku akisisitiza kuwa nawahakikishia wapambanaji wote na wananchi wote wa Iraq kuwa, haki iko pamoja nanyi, walimwengu wote wanaopenda haki wako pamoja nanyi huku wakisubiri ushindi wenu dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Kukombolewa mji wa Tal Afar hususan kunahusu wakazi wa mji huo na wananchi wote wa Iraq bila kujali kabila lolote na imani na kaumu yoyote, kwani ni mali ya kila Muiraq, sawasaw awe Muislamu au Mkristo, Muizad au Mkurdi hivyo tunapaswa kushikamana katika kuijenga Iraq ya wote.  

mwishp/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky