Watu 30 wauwawa kufuatia shambulio la majeshi ya Marekani

  Watu 30 wauwawa kufuatia shambulio la majeshi ya Marekani

Mashambulizi ya ndege za anga za umoja wa kukabilia na Magaidi Daesh chini ya usimamizi wa Marekani, wamefanya mashambulzi katika mkoa Haskah nchini Syria ambayo yamesababisha mauaji ya kuuwawa wananchi 30 wasiokuwa na hatia.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: chanzo kimoja muhimu nchini Syiria kimetangaza kuwa wananchi 30 wameuwawa kufuatia shambulio la ndege za kivita za umoja wa mataifa chini ya usimamizi wa Marekani, yaliofanywa katika mkoa wa Haskah nchini Syria ambapo asilimia kubwa ya waliofariki ni wanawake.
Kwa mujibu wa ripoti hii watu wengine 20 wamejeruhiwa kufuatia shambulio hilo, huku zikiashiriwa kusababisha hasara kubwa ya kuaharibu makazi ya wananchi hao.
Umoja wa kukabiliana na kikundi cha kigaidi cha Daesh kinacho simamiwa na Serikali ya Marekani, kimeshambulia sehemu hiyo kwa mashambulizi ya anga, katika hali sehemu ziliokuwa zimeshambuliwa hakuna makazi ya magaidi hao, ambapo inadaiwa kuwa vikundi vya kigaidi vya Daeshi vinadaiwa kuwepo mbali na sehemu hiyo nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky