Mauaji ya kinyama dhidi ya mashia wa kijiji kimoja nchini Nigeria+ picha

Mauaji ya kinyama dhidi ya mashia wa kijiji kimoja nchini Nigeria+ picha

Makumi ya wakazi wa kijiji cha Guwasika kiliopo katika wilaya ya Kaduna nchini Nigeria wameuwawa kufuata shambulio liliofanywa na watu wauvu wasiojulikana nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mkuu wa jeshi la Polisi katika wilaya ya Kaduna nchini Nigeria ametangaza kuuwawa kwa uchache watu 45 na wengine kujeruhiwa kufuatia shambulio liliofanywa na watu wasiojulikana katika kijiji cha Guwasika.
Kaduna ni mkoa ambao unawakazi wengi sana ambao ni wafuasi wa madhehebu ya Shia ambao wako chini ya usimamizi wa Sherikh Ibrahim Zakizakiy katika sehemu hiyo, kijiji kilichotajwa kinasadikiwa kuwepo kwa wezi na majambazi ambao huiba kwa kutumia silaha.
Ripoti zinaashiria kuwa miongoni mwa waliofariki ni watoto waliochini ya miaka kumi, huku ikielezwa kuwa baadhi ya miili imeonekana imekatwa viungo.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa: watu hao walivamia kijiji hicho katika nyakati za Alasiri na kukizingira kijiji hicho, kisha wakaanza kuchoma moto nyumba za kijiji hicho huku wakiwatupia risasi wananchi hao na kupelekea kuuwawa kwa wananchi hao nchini humo.


mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky