Mbunge wa bunge la Marelkani: Saudi Arabia ni katika mataifa makubwa yanayosaidia magaidi

Mbunge wa bunge la Marelkani: Saudi Arabia ni katika mataifa makubwa yanayosaidia magaidi

Mbunge mmoja katika Bunge la Marekani ameashiria hali ya kukinzana ya taifa lake katika kuiunga mkono serikali ya Saudi Arabia pamoja yakuwa nchi hiyo kuwa kinara wa kusaidia vikundi vya kigaidi, bado Marekani inaendelea kukuza uhusiano wake na nchio hiyo, jambo ambalo linapingana na madai yake ya kupambana na ugaidi

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Mbunge mmoja katika Bunge la Marekani ameashiria hali ya taifa lake kuiunga mkono serikali ya Saudi Arabia pamoja yakuwa nchi hiyo kuwa kinara wa kusaidia vikundi vya kigaidi, lakini bado marekani inakuza fungamano lake na nchio hiyo jambo ambalo linapingana na kudai kwake linapamana na ugaidi.
Mbunge mmoja wa Bunge la Marekani (Tulsi Gabard) ameyasema hayo  alipokuwa anaojiwa na Televishen ya CNN na kusisitiza kwa kuisifu Saudi Arabia kuwa ni taifa linalosaidia zaidi magaidi kuwa: Saudi Arabia ni moja kati ya mataifa makubwa yanayosaidia vikundi vya kigaidi kama vile Alkaida na Daesh, lakini jambo la ajabu na kushangaza ni kuona serikali ya Marekani bado linaendelea kukuza fungamano lake na taifa hilo huku ikidai kuwa inapambana na vikundi vya kigaidi duniani jambo ambalo linatia mashaka na kuleta mkizano.
mwsho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky