Mfalme wa Kuwait atoa pongezi kwa ushindi wa serikali ya Iraq dhidi magaidi katika mji wa Musol

Mfalme wa Kuwait atoa pongezi kwa ushindi wa serikali ya Iraq dhidi magaidi katika mji wa Musol

Mfalme wa Kuwait na waziri mkuu wake, ikiwa kila mmoja katika nyakati tofauti wametuma ujumbe kwa Rais wa Iraq na waziri mkuu wa nchi hiyo kwa mnasaba wa kukombolewa kwa mji wa Musol kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Sheikh Sabahi Al-ahmad ambaye ndio mfalme wa Kuwait ametuma ujumbe wa pongezi kwa Rais wa jamhuri ya Iraq na waziri mkuu wa nchi hiyo “Haidar Al-abadi” kwa mnasaba wa kukombolewa kwa mji wa Musol kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo, huku akiombea nchi hiyo irudi katika hali yake ya zamani ya amani na utulivu.
Mfalme huyo katika ujumbe huo amesema kuwa kukisambaratisha kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Musol ni mafanikio makubwa kwa serikali ya Iraq, huku akisisitiza kuwa serikali ya Kuwait inaunga mkono juhudi zinazochukuliwa na serikali ya Iraq katika kuhakikisha taifa hilo linapata amani na utulivu na kuwasambaratisha magaidi katika taifa hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ziliotufikia ni kwamba inasemekana wizara ya ulinzi na usalama nchini Iraq imetangaza siku ya Alhamisi 29 mwezi sita wizara hiyo ilitangaza kauli ya kukoma kwa utawala wa kikundi cha Daesh katika mji wa Musol, mji ambao ndio makao makuu ya utawala wa kigaidi wa Daesh nchini humo.

mwesho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky