Miili 21 yagunduliwa nchini Misri baada ya miaka 2 kuchinjwa na magadi wa Daesh+ picha

Miili 21 yagunduliwa nchini Misri baada ya miaka 2 kuchinjwa na magadi wa Daesh+ picha

Miili 21 ya wakristo wa Misri waliokuwa wanaishi kusini mwa mji wa Sirte nchini Libya imeonekana ambayo iliuliwa na magaidi wa kgaidi wa Daesh nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: idaara ya kukabiliana na vitendo vya kigaidi katika mkoa wa Misurata nchini Libya leo imesambaza picha za miili ya wakristo 21 wa Misri walikuwa wameuliwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Sirte kusini mwa Libya.
Kuonekana kwa miili hiyo kumetokea baada ya magaidi kadhaa kutekwa na majeshi ya Libya na baada ya kuhojiwa walienda kuonyesha sehemu waliokuwa wamewafukia baada ya kuwachinja.
Ofisi ya kupambana na jinai za kigaidi katika mkoa wa Misurata imetoa ripoti yake ikesema kuwa: miili hiyo waliikuta kuwa kabla ya kuuliwa ilikuwa imefungwa mikono kwa nyuma na baadae waliwakata vichwa vyao.
Kwa upande mwingine miili ya wakristo hao imechukuliwa kupelekwa makao makuu ya Misurata kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya kufahamika majina yao.
Inasemekana kwamba kikundi cha kigaidi cha Daesh kiliwateka wakristo 21 wa Kibtiy mnamo mwanzoni mwaka 2015 ambapo walifunga mikono kwa nyuma na kuwanyonga katika fukwe za kusini mwa mji mkuu wa Libya, ambapo baada ya kusambazwa kwa mauaji hayo kupiatia magaidi hao, jumuia za kimataifa zililaani vibaya sana mauaji hayo ya kikatili.   

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky