Misri: sitachukua hatua yeyote dhidi ya Hizbullah nchini Lebanon

Misri: sitachukua hatua yeyote dhidi ya Hizbullah nchini Lebanon

Rais wa Jamhuri ya Misri ametoa kauli akijibu umbi la utawala wa Saudi Arabia la kutaka kukiwekea vikwazo kikundi hicho amesema: Misri haitachukua hatua yeyote dhidi ya kikundi cha Hizbullah na wala haifikiri kufanya hivyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Abdel Fattah El-sisi aliyasema hayo baada ya ombi kutoka serikali ya Saudi Arabia lakumtaka washirikiane katika kuiwekea vikwazo Hizbullah amesieitiza kwa kusema: serikali ya Misri haitachukua hatua yeyote dhidi ya kikundi hicho nchini Lebanon.
Rais wa jamhuri ya Misri ametangaza rasmi mtazamo wake kuwa sisi hatuna mpango wowote wa kukabiliana na Hizbullah na tunaonga mkono kuendelea kwa uimara na amani nchini humo.
Aidha alipokuwa anajibu swali hili kuwa je Misri itachukua hatua yeyote katika kukabiliana na kikundi cha Hizbullah, alisema suala la kikundi cha Hizbullah hakina uhusiano wowote wa kukiwekea kikwazo au kutokiwekea kikwazo, huku akibainisha kuwa mazingira ya ukanda wa mashariki ya kati hali mbaya ambapo tufanya juhudi ya kupata amani maeneo yalikuwa hayana amani kama vile Iraq, Syria, Libya, Yemen na Somalia, ambapo tunapaswa kuwasaidia waweze kupata amani na utulivu.
Huku akimalizia kwa kusema kuwa ukanda wa mashariki ya kati umechoka kuona marumbano na machafuko ya kitaifa hivyo tunapaswa kutumia busara katika kutatua matatizo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky