Mji wa Dawaseh magharibi mwa Musol wakombolewa+ picha

 Mji wa Dawaseh magharibi mwa Musol wakombolewa+ picha

Majeshi ya Polisi ya Iraq na majeshi mengine nchini humo leo wamefanikiwa kuikomboa sehemu ya Dawaseh kikamilifu kutoka kwa kikundi cha kigaidi cha Daesh na kuisimika bendera ya Iraq katika majengo ya sehemu hiyo

Shirika la habari AhluBayt (a.s) ABNA: kamanda wa mashambulizi ya kuukomboa mji wa Musol ametangaza kukombolewa kikamilifu sehemu ya Dawaseh iliopo magharibi mwa Musol, ambapo kukombolewa kwa sehemu hiyo kumekamilika siku ya Jumanne nchini humo.
Kamanda mkuu wa mashambulizi hayo Abdul-Amiri Yarallah katika kauli yake ametangaza kuwa, majeshi ya Polisi ya Ira yakishirikiana na majeshi mengine ya nchi hiyo, wamefanikiwa kuikomboa sehemu ya Dawaseh kikamilifu kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo baada ya kuikomboa sehemu hiyo walichomeka bendera ya Iraq katika majengo makubwa ya sehemu hiyo.
Aidha amefafanua kwa kusema kuwa katika mashambulio ya kuikomboa sehemu hiyo, majeshi ya Iraq yameingiza hasara kubwa kwa vikundi vya kigaidi vya Daesh ikiwemo kuangamia kwa idadi kubwa ya magaidi na kusambaratishwa kwa vifaa vyaoo vya kivita katika sehemu hizo.
Sehemu ya Dawaseh ni katika sehemu za muhimu upande wa magharibi mwa Musol, ambapo sehemu hiyo ndio kulikuwa na msikiti mkubwa ambao Khalifah wa kikundi cha kigaidi cha Daesh alikuwa akitoa hutuba na kauli zake katika msikiti huo.
Pia masaa kadhaa yaliopita kamanda wa mashambulizi ya kuikomboa Musol ametangaza kuwa sehemu ya Tal Raman tayari imekombolewa na majeshi ya Iraq hivi karibuni, hku majeshi ya Iraq hivi sasa yako katika harakati ya kuingia katika sehemu hiyo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky