Mke wa Mufti wa Daesh ajichoma moto yeye na watoto wake watatu nchini Iraq

Mke wa Mufti wa Daesh ajichoma moto yeye na watoto wake watatu nchini Iraq

Kwa mujibu wa maelezo ya chanzo kimoja cha habari katika mji wa Tal Afar nchini Iraq; mke wa Mufti wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Tal Afar amejinyoga kwa kujichoma moto yeye akiwa na watoto wake watatu nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mke wa Mufti wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Tal Afar, mji ambao uko mbali na mji wa Musol kwa kilometa 60 nchini Iraq, amejinyonga m, mama huyo kwa kujichoma moto yeye akiwa na watoto wake watatu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari viliotangaza habari hii, ni kwamba mpaka sasa sababu ya kufanya tukio hilo la kusikitisha bado haijafahamika, pamoja yakuwa wengi wanasema kuwa suala hilo linaambatana na masuala ya kushindwa mara kwa mara kwa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika sehemu mbalimbali nchini Iraq.

Mji wa Tal Afar kwa sasa ndio umeanishwa kuwa ni makao makuu ya kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq, baada ya kikundi hicho kushindwa na kusambaratishwa katika mji wa Musol nchini Iraq, ambapo mji wa Tal Afar uko umbali wa kilometa 60 magharibi mwa mji wa Musol nako ndiko walipokusanyika magaidi waliokimbia Musol na sehemu nyingine za miji ya Iraq.

 mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky