Mkuu wa jeshi la usalama wa taifa aenguliwa nchini Saudi Arabia

Mkuu wa jeshi la usalama wa taifa aenguliwa nchini Saudi Arabia

Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimetanga kuenguliwa kwa “Mutibu bin Abdallah” ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa jeshi la ulinzi na usalama wa taifa nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Salmani bin Abdilazizi ”mfalme wa Saudi Arabia” usiku wa Jumamosi ametoa amri ya kuwaengua viongozi kadhaa wa usalama wa taifa na kuwainisha wengine watakaoshika nyadhifa hizo.
“Mutibu bi Abdallah” mtoto  wa mfalme aliopita wa Saudia ambaye alikuwa ni mkuu wa majeshi ya usalama wa taifa hilo ameenguliwa katika nafasi hiyo kwa amri ya mfalme Salmani.
Kwa upande mwingi Mfalme wa Saudi Arabia amemuanisha “Khalidi bin Ayafi” kuwa atashika  nafasi ya Mutibu bin Adillah, hivyo Khalidi bin Ayafi kuanzia sasa ndiye atakuwa kiongozi mkuu wa jeshi la usalama wa taifa la Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa amri ya Mfalme wa Saudi Arabia “Adili Faqiih” ameenguliwa katika nafasi yake ya waziri wa uchumi ambapo wizara hiyo amepewa Muhammad Tuwayjiri nchini humo.
Aidha Mfalme wa Saudi Arabia ametoa amri ya kustafu kwa mkuu na kamanda wa jeshi la maji nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky