Mkuu wa majeshi ya Iran awasili mjini Ankara Uturuki

Mkuu wa majeshi ya Iran awasili mjini Ankara Uturuki

Kiongozi mkuu wa majeshi nchini Iran akiwa pamoja na makamanda wa jeshi la Ardhi wawasili Ankara mji mkuu wa serikali ya Uturuki

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Kiongozi mkuu wa majeshi nchini Iran akiwa pamoja na makamanda wa jeshi la Ardhi wawasili Ankara mji mkuu wa serikali ya Uturuki.
Aidha kiongozi huyo amewasili nchini humo baada ya witu maalumu kutoka kwa mkuu wa majeshi ya serikali ya Uturuki, ambapo ataonana na viongozi wakuu wa nchi hiyo, ikiwemo viongozi wa kisiasa na kijeshi kama vile mkuu wa majeshi ya Uturuki na waziri wa ulinzi na usalama wa serikali ya Uturuki, ambapo wataonana na kuzungumzia mambo mablimbali ya pande mbili za nchi hizo.
Katika safari hiyo pia mkuu wa majeshi ya Iran ataonana na Rais wa nchi hiyo (Rajab Tayib Ardugan) na kuzungumzia mambo mbalimbali muhimu kati ya mataifa hayo.
Mambo muhimu yatakayo zungumziwa katika safari ya mkuu wa majeshi ya Iran na kiongozi mwenza wa Uturuki ni pamoja na hali ya mabadiriko ya ukanda wa mashariki ya kati, jinsi ya kukabiliana na vikundi vya kigaidi, ushirikiano wa mipaka ya nchi hizo mbili ambapo ndio mambo muhimu ambayo watakayo yazungumzia kati safari hiyo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky