Mkuu wa polisi akamatwa kwa kwa tuhuma dhidi ya waziri mkuu Ethiopia

Mkuu wa polisi akamatwa kwa kwa tuhuma dhidi ya waziri mkuu Ethiopia

Idadi ya waliokufa kutokana na shambulizi la guruneti kwenye mkutano wa hadhara katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, imefikia watu wawili.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Idadi ya waliokufa kutokana na shambulizi la guruneti kwenye mkutano wa hadhara katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, imefikia watu wawili.

    

Watu 30 wamekamatwa kuhusiana na mlipuko huo wakiwemo polisi kadhaa, akiwemo naibu kamishna wa polisi wa Addis Ababa.

Shambulizi hilo lilitokea katika uwanja mkubwa wa wazi uliokuwa umefurika, wakati Waziri Mkuu Abiy Ahmed akikamilisha hotuba yake mbele ya maelfu ya watu siku ya Jumamosi.

Vurugu zilizozuka baada ya mripuko huo wakati watu walianza kukimbilia jukwaani ziliwajeruhi watu 150.

Hakuna aliyetangaza kuhusika na shambulizi hilo lisilo la kawaida katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ambao kila mara huwa na ulinzi mkali.

Ethiopia imesema kuwa Marekani itawatuma wapelelezi wa FBI ili kusaidia kuchunguza shambulizi hilo.

Mwisho wa habari/ 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky