Mmoja katika washakiwa 15 wa mauaji ya Khashoggi afariki kwa ajali ya kutatanisha

 Mmoja katika washakiwa 15 wa mauaji ya Khashoggi afariki kwa ajali ya kutatanisha

Mmoja miongoni mwa watuhumiwa 15 ambao siku aliopotea Jamali Khashoggi “mwandishi wa Saudi Arabia” alikuwepo katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia ambapo ndio sehemu aliokuwa amepotelea muandishi aliyekuwa anaikosoa serikali ya Saudi Arabia, amefariki katika tukio la kutatanisha la ajali ya gari nchini Sauadi Arabia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Mmoja miongoni mwa watuhumiwa 15 ambao siku aliopotea Jamali Khashoggi “mwandishi wa Saudi Arabia” alikuwepo katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia ambapo ndio sehemu aliokuwa amepotelea muandishi aliyekuwa anaikosoa serikali ya Saudi Arabia, amefariki katika tukio la kutatanisha la ajali ya gari nchini Sauadi Arabia.
Aidha kutokana na tukio la kufariki kijana huyo ambaye ni mwanajeshi wa jeshi la Saudi Arabia ambaye alikuwepo katika ubalozi aliopotelea Jamali Khashoggi siku aliopotea muandishi hoyo, ambapo wahariri wanasema kuwa mwanjeshi huyo ameuliwa ili isije kutoa siri ya mauaji ya muandishi aliokuwa anaukosoa utawala wa Saudi Arabia.
Albustani aliingia nchini Uturuki Asubuhi ya saa 11:45 kwa sehemu hiyo ambayo ilikuwa ni terehe 2 mwezi wa kumi na aakakodi chumba katika Hoteli moja aliopo mjini humo na aliondoka siku hiyohiyo mnamo usiku wa saa tatu na dakika arubani na sita kwa kutumia Jeti maalumu ya shirika la ndege la Saudi Arabia na kurudi nchini Saudi Arabia.
Kwa upande mwingine Jamali Khashoggi aliingia katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia asubuhi ya tarehe hiyo na baada ya kuingia hakuwa ametoka tena katika ubalozi huo, jambo ambalo baadhi ya viongozi nchini Uturuki wamesema kuwa muandishi huyo ameuliwa baada ya kuingia katika ubalozi huo.
Dhana ya kuhusika kwa mwanajeshi huyo na tukio la kuuwawa kwa muandishi huyu, imeshadidi zaidi baada ya taarifa ya kufariki kwa mwanajeshi hiyo katika tukio la ajali ya kutatanisha nchini Saudi Arabia.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky