Mogherini: Iran imetekeleza ahadi yake ya makubaliano ya Nyuklia

Mogherini: Iran imetekeleza ahadi yake ya makubaliano ya Nyuklia

Kiongozi wa masuala ya siasa za mambo ya nje katika umoja wa Ulaya ametoa ujumbe wake ikiwa kama jawabu la hutoba ya Rais wa Marekani Donald Trump

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Federica Mogherini alitoa ujumbe huo baada ya hutuba ya rais wa Marekani kuhusu makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran na kusema kuwa: makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran ni makubaliano yalifanywa na pande kadhaa chini ya maazimio ya shirika la usalama la umoja wa Mataifa, ambapo makubaliano ya nyuklia ya Iran yanatoa dhamana ya kwamba Iran haitatumia nishati hiyo kwaajili ya masuala ya kijeshi.
Aidha aliongeza kusema kuwa: serikali ya kiislamu ya Iran mpaka sasa imetekeleza ahadi zake zilizokuwa zinahitajika toka kwake katika makubaliano hayo, huku akisisitiza kuwa muafaka wa mpango wa nyuklia wa Iran ni moja katika ya nguzo za asili za kuzuia uzalishaji wa nyuklia, ambapo sote kwa pamoja tunawadhifa wa kuyalinda makubaliano haya kwaajili ya usalama na amani na kwa manufaa yetu sote.
Federica Mogherini amesisistiza kuwa, kwa upande wa umoja wa Ulaya bilashaka ikowazi na tumeshasema kwa wazi kuwa Makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran daima tutauhami na utaendelea kubaki kama tulivyo kubaliana.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky