Mogherini: Umoja wa Ulaya utaenedelea kushikamana na mapango wa nyuklia wa Iran

Mogherini: Umoja wa Ulaya utaenedelea kushikamana na mapango wa nyuklia wa Iran

Msimamizi wa masuala ya siasa za mambo ya nje katika umoja wa Ulaya amesema: tutaenedelea kushikana na makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Federica Mogherini baada ya Trump kutangaza rasmi ya kujitoa kwake katika makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran na kuahidi kuweka vikwazo vingine vizito vya uchumi dhidi ya Iran, alisema kuwa: umoja wa Ulaya kila mara umekuwa wenye kutangaza kuwa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Iran imesababisha kupatikana fungamano zuri la kibiashara na uchumi kati ya Iran na jumuia ya umoja wa Ulaya, huku akisisitiza kuwa umoja wa Ulaya utaendelea kushikamana na makubaliano hayo.
Aidha aliendelea kusema kuwa: makubaliano ya mpango wa nyuklia kati ya Iran na kikundi cha 5+1 yamefikiwa baada ya juhudi za kidiplomasia ziliofikiwa baada ya miaka 12, makubaliano ambayo faida yake zinarudi kwa walimwengu wote, nayo yameifanya  isiweze kufikia lengo lake la kumiliki silaha za Nyuklia.
Naye alimalizia kwa kusema huku akiwa mwenye huzuni kuwa tutaendelea kuyalinda makubaliano ya mpango wa nyuklia ya Iran kwaajili ya kutaka amani usalama wa ulimwengu.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky