Moscow: hakuna sababu za msingi za kufanya ukaguzi wa vituo vya kijeshi vya Iran

Moscow: hakuna sababu za msingi za kufanya ukaguzi wa vituo vya kijeshi vya Iran

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imetangaza kuwa: wamarekani wanapaswa wapetie upya vipengele vya makubaliano ya Nyukilia na Iran, ili wafahamu vizuli vipengere vya makubaliano hayo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya mambo ya nje ya Urusi imetangaza kuwa: hakuna sababu za msingi za kupelekea Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, kutaka kuchunguza maeneo ya kijeshi ya serikali ya jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Wizara hiyo iliyasema hayo katika kupinga maelezo ya mwakilishi wa Marekani katika umoja wa Mtaifa na kusisitiza kuwa, kwa masikitiko makubwa serikali ya Marekani inamtazamo wakuwa, Urusi inaihami serikali ya Iran na hairuhusu shirika la Nishati la Umoja wa mataifa kwenda kufanya uchunguzi katika maeneo ya kijeshi nchini Iran.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi alimalizia maelezo yake kwa kusema kuwa: tunawanasihi ndugu zetu  wamarekani kuwa wanapaswa wapetie upya vipengele vya makubaliano ya mpango wa Nyukilia uliofanyika kati ya Iran na jumuia ya 5+1, ili wafahamu vizuli vipengere vya makubaliano hayo pia kuepuka kutaka mambo yaliokuwa kinyume na makubaliano.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky