Mpango mbaya wa Daesh wa kushambulia sehemu takatifu na nyumba ya kiongozi wa dini wa Iraq wateketezwa kabla ya kutekelezwa

Mpango mbaya wa Daesh wa kushambulia sehemu takatifu na nyumba ya kiongozi wa dini wa Iraq wateketezwa kabla ya kutekelezwa

Timu ya uchungu na ujasusi iliokuwa chini ya wizara ya ulinzi na usalama nchini Iraq imefanikiwa kufichua mpago mbaya zaidi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh wa kushambulia maeneo matakatifu yaliopo nchini Iraq ikiwemo kuripua nyumba ya kiongozi mkubwa wa dini nchini humo Ayatullah Sistaniy

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya ulinzi na usalama nchini Iraq vimetangaza kufichua mpango mkubwa wa kikundi cha Kigaidi cha Daesh wa kushambulia miji mitakatifu na nyumba ya kiongozi mkuu wa Dini nchini Iraq, ambapo kufuatia kusambaratisha kwa mpango huo makumi ya magaidi hao wameangamia.

“Abu Ali Albasariy” kiongozi wa sekta ya usalama inayofungamana na wizara ya ulinzi na usalama nchini Iraq amesema: mpango huo ulifichuka baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na vijana wetu, kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh kinalengo la kufanya mashambulio makubwa matatu kwa pamoja katika miji mitatu chini ya usimamizi wa makamanda wao kutoka mataifa ya nje, ikiwemo miripuko ya kujitolea muhanga na magari yaliotegwa mabomu, katika mji wa Karbala,    Najaf, Samarra, Kufah, Kufah na nyumba ya kiongozi mkuu wa dini Ayatullah Sistaniy, ambapo kabla ya kutekelezwa mashambulizi hayo mpango huo ulifichuliwa na kusambaratishwa kikamilifu.

Aidha ameongeza kusema kuwa baada ya kufahamika mpango huo mchafu taarifa ziliwasilishwa kwa waziri mkuu wa nchi hiyo na baada ya waziri mkuu huyo kutoa maamuzi ndege za kivita za Iraq zilishambulia sehemu mbili walizokuwa wanakutana magaidi hao kwaajili ya kufanya jaribio lao hilo katika sehemu ya Almayadin iliopo Syria na Alqaim nchini Iraq, huku akibainisha kuwa mashambulio mengine yalifanywa katika sehemu 7 ziliopangwa kutekelezwa kwa mpango na kuziangamiza kikamilifu ambapo makumi ya magaidi waliangami katika mashambulio hayo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky