Msemaji wa jeshi la anga nchini Yemen: wawekezaji wa kigeni waliopo Emirates na Saudia waondoke haraka nchini humo

Msemaji wa jeshi la anga nchini Yemen: wawekezaji wa kigeni waliopo Emirates na Saudia waondoke haraka nchini humo

Msemaji mkuu wa majeshi ya anga ya Yemen ametoa ujumbe kwa mashirika yote yaliokuwepo Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Emirates) kuendelea kufanya harakati zao za kiuchumi katika nchi hizo, huku akisisitiza kuwa wafanya biashara wote waliopo katika mataifa hayo wanapaswa kuondoka katika mataifa hayo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na msemaji mkuu wa jeshi la anga la nchini Yemen mjini Sana`a kuwa maeneo yote ya taifa la Emirates yanaweza kushambuliwa na majeshi ya Yemen.
Aidha amesema alipokuwa anahojiwa na Televishen ya Aljazirah na kusisitiza kuwa tuna ushahidi wakutosha unaonyesha kufanikiwa kwa shambulio tuliolifanya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai liliofanywa na ndege za kivita zisizokuwa na rubani.
Mwisho amemaliza kusema kwa kuyataka mashirika yaliowekeza na kufanya shughuli zake za kiuchumi nchini Saudi Arabia na Emirates kusitisha harakati hizo nchini humo na kuondoka katika nchi hizo ili waseje wakapata hasara kufuatia mashambulizi ya anga yatakayofanywa na majeshi ya Yemen katika mataifa hayo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky