Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani: tunafuatilia kwa kina mpango wa makombora ya Iran

 Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani: tunafuatilia kwa kina mpango wa makombora ya Iran

Msemaji mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema: daima tumekuwa tukifuatilia kwa kina mpango wa makombora ya masafa marefu ya serikali ya kiislamu ya Iran

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani na kusisitiza kuwa tuko katika kufuatilia kwa umakini mkubwa mpango wa makombora ya masafa marefu ya serikali ya kiislamu ya Iran kwa undani na uakribu zaidi.
Aidha alisema alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kuwa: sisi  katika wizara ya mambo ya nnje tupo katika kufuatilia suala hili kwa kina zaidi, hivyo basi tutaendelea kufanya hivyo katika kufuatilia mpango wa makombora ya masafa marefu ya Iran kwa umakini zaidi hata kujua mwisho wake.
Aidha katika kuendelea kuzungumzia hilo alijizuia kufafanua zaidi kadhia hiyo kutokana na uchache wa muda, hivyo alihitimisha kikao hicho na kutoa kauli ya kuandaa kikao kingine atakachokiita hapo baadae na kufafanua suala hilo kwa kina zaidi.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky