Mufti wa Daesh atoroka Musol kwa kutoa rushwa

Mufti wa Daesh atoroka Musol kwa kutoa rushwa

Mufti wa kikundi cha kigaidi cha Daesh afanikiwa kutoroka mjini Musol baada ya kutoa rushwa kwa majeshi ya usalama wa sehemu hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: gazeti la Saudi Arabia la Ukadh likinukuu kutoka kwa Zuhairi Ajaburiy kutoka kwa makamanda wa Musol kuwa wametoa ripoti kuwa, Mufti wa Daesh anaefahamika kwa jina la Abu-omari kuwa ametoa rushwa kwaajili kutoroka sehemu hiyo.
Aljaburiy amebaisha kuwa: mufti huyo wa kikundi cha kigaid cha Daesh alikamatwa nje ya mji wa Musol ambapo baada ya kukamatwa kwake alitoa rushwa ya dola elfu 7 na kufanikiwa kutoroka katika mji huo.
Aidha ameashiria kuwepo suala la rushwa baina ya majeshi ya usalama ya Iraq, huku akisema kuwa, suala la rushwa lilikuwa limeenea kwa kiasi kikubwa, ama hivi sasa limepungua kwa kiasi kikubwa sana, ambapo baadhi ya magaid wa Daesh wamefanikiwa kutoroka nchini humo kwakutoa rushwa.
Mufti huyo alikuwa ndiye mtoa hukumu katika maeneo yalikuwa yametekwa na magaidi wa Daesh alikamatwa siku ya Jumamosi na majeshi ya ulinzi ya nchi hiyo.
Abu-omar ni katika magaidi maarufu wa Daesh kipindi ambacho kikundi hicho kilikuwa kimeuteka mji wa Musol ambaye alikuwa hukumu za kuuliwa wananchi wa Musol naye alikuwa ndiye msomaji wa hukumu iliokuwa imetolewa dhidi ya wananchi na kuitekeleza.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky