Mugherini: ni changamoto kubwa kuhifadhi mpango wa Nyuklia na kurejeshwa vikwazo vya Marekani

Mugherini: ni changamoto kubwa kuhifadhi mpango wa Nyuklia na kurejeshwa vikwazo vya Marekani

Msimamizi wa siasa za nje katika umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa kuhifadhi makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran ni kwa manufaa ya mataifa ya umoja huo, huku akisema kuhifadhi makubaliano hayo pamoja na kurejeshwa kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran ni changamoto nzito

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Federica Mogherini, kiongozi wa masuala ya siasa za mambo ya nje katika umoja wa Ulaya amesema hayo alipokuwa ameonana na Rais wa Austria katika mji wa Vienna, na kusisitiza kuwa umoja wa Ulaya unaendeleza juhudi zake za kuhifadhi makubaliano ya mpango wa Nyuklia.
Aidha alisema kuwa bado tunaendelea kushauriana kuhusu suala la kuhifadhi makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran, makubaliano ambayo ylipatikana baada ya vikao vingi vilivyofanyika katika mji wa Vienna na kufikia tija ya makubaliano hayo, hivyo tunapaswa kuhifadhi na kulinda msingi na asili ya makubaliano hayo, kwani kuhifadhi makubaliano hayo ni kwa manufaa ya usalama wa umoja wetu.
Kadhalika amsema kuhifadhi mpango wa Nyuklia baada ya maamuzi ya Marekani ya kurejesha vikwazo dhidi ya Iran, ni changamoto kubwa sana kwetu, ama bado tunaendelea kufanya juhudi za kufanya mazungumzo na mataifa mbalimbali na washirika wetu ulimwenguni kwaajili ya kuendelea kuhifadhi makubaliano ya mpango wa Nyukilia.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky