Muislamu auliwa nchini India kwa sababu ya kununua Ng`ombe

Muislamu auliwa nchini India kwa sababu ya kununua Ng`ombe

Polisi nchini India imetangaza habari ya kuuwawa kwa Muislamu mmoja na wafuasi wa dini ya Hinduu, kutokana na kwamba Muislamu huyo alikuwa akifanya biashara ya Ng`ombe

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jeshi la Polisi nchini India imeeleza kuwakamata waliomuuwa Muislamu mmoja nchini humo, kupitia wafuasi wa dini ya kihinduu nchini humo.
Majeshi ya usalama ya India siku ya Ijumaa yaliukuta mwili wa marehemu Umari Khan aliokuwa na umri wa miaka 35, ambaye ni muumini wa dini ya Kiislamu nchini humo, kuwa umelazwa katika leri la treni katika mji wa Alwar mkoa wa Rajasthan kaskazini mwa magharibu mwa nchi hiyo.
Kamanda wa jeshi la Polisi katika mji wa Alwar amesema: Muislamu huyo ameuliwa kwakile kinachoadaiwa kuwanusuru Ng`ombe, ambapo baada ya uchungu imebainika kuwa, Muislamu huyo alikuwa akifanya biashara Ng`ombe ambayo hairuhusiwi kufanya katika sehemu hiyo.
Aidha alieleza kuwa marehemu alipokuwa amebeba Ng`ombe watano katika gari yake, alionekana na wauwaji hao ndipo watu 6 kutoka katika kikundi kinadaiwa cha kuwanuru Ng`ombe wakamshambulia hata kumuua.
Inasemekana kuwa mnyama aina ya Ng`ombe katika dini ya Kihindu ni myama mtakatifu, akatika sehemu nyingi nchini humo imezuiliwa kumua myama huyo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky