Mwanasheria mkuu wa Marekani atuhumiwa kuingilia uchaguzi

Mwanasheria mkuu wa Marekani atuhumiwa kuingilia uchaguzi

Rais wa Marekani Donald Trump ameingia tena katika msukosuko mwengine wa kisiasa baada ya kubainika Mwanasheria mkuu Jeff Sessions kudaiwa kufanya mazungumzo na balozi wa Urusi nchini Marekani wakati wa kampeni.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Marekani Donald Trump ameingia tena katika msukosuko mwengine wa kisiasa  baada ya kubainika Mwanasheria mkuu Jeff Sessions  kudaiwa kufanya mazungumzo na balozi wa Urusi nchini Marekani wakati wa kampeni.

Mawasiliano hayo yamezusha wito katika bunge la Marekani la kumtaka kujiondoa katika uchunguzi unaofanywa na wizara ya sheria juu ya Urusi kuuingilia uchaguzi wa Marekani ulimwingiza madarakani Trump.

Sessions, ambae ni muungaji mkono wa mwanzo kabisa wa Rais Donald Trump na mshauri wa kisera wa mgombea wa chama cha Republican, hakuwaweka wazi kile walichozungumza na balozi huyo wa Urusi wakati shauri hilo liliposikilizwa  mwezi uliopita pale alipoulizwa atafanya nini pale yeyote akibainika katika kampeni ana mawasiliano na maafisa wa Urusi. Mwanasheria huyo mkuu alijibu hajafanya mawasiliano na Warusi.

Jumatano usiku msemaji wa wizara ya sheria Sarah Isgur Flores alisema alisema kwa hakika hakuna kilichopotoshwa katika majibu yake hayo. Taarifa hiyo haikukidhi matakwa ya Wademokrat, ambao kabla ya siku hiyo walishinikiza kiongozi huyo ajiondoe katika muendelezo wa uchunguzi na kuzusha maswali ya uwezekano wa kusimamia vyema uchunguzi.

Kauli ya kiogozi wa upinzani bungeni

Kiongozi wa chama cha Demokratik katika bunge la Marekani Nancy Pelosi amemtuhumu Sessions kwa kuongopa pamoja na kula kiapo na akataka ajiuzulu. Wademokratik wengine wamepiga kelele za kutaka ajiweka kandoni na uchunguzi huo. 

Katika taarifa yake Ijumaa jioni, Sessions alisema hajawahi kukutana na afisa yeyote wa Urusi kujadili suala la kampeni. Hana fikra zozote kuhusu tuhuma hizo. Na kuongeza kuwa ni upotoshaji. Lakini kitengo cha uchugzi kimethibitisha kuwa, akiwa kama Seneta wa Marekani na mwanachama mwandamizi wa kamati ya bunge ya huduma za silaha, mwanasheria huyo mkuu anatajwa kufanya zaidi ya majadiliano 25 na mwaka jana, na amefanya mazungumzo mengine mara mbili tofauti na balozi wa Urusi Sergey Kislyak.

Moja katika mikutano hiyo ulifanyika Septemba akiwa Seneta, sambamba na mikutano mingine na wajumbe wa Uingereza, Chuina, Ujerumani na mataifa mengine. Mwengine ulifanyika kwa makundi baada ya hotuba ya hafla maalumu ya Wakfu wa Urithi, ambayo mtuhumuwa aliitoa katika kipindi cha kiangazi. Hafla hiyo ilijumuisha mabalozi kadhaa akiwemo wa Urusi. Balozi huyo anatajwa alikwenda moja kwa Sessions baada ya kuzungumza wakati anaondoka katika jukwaa. Habari hizo za mawasiliano, kwanza kabisa  ziliandikwa na gazeti la Washington Post.

Mwisho wa habari / 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky