Ndege za kivita za Iraq zashambulia makamanda wa Daesh nchini Syria

Ndege za kivita za Iraq zashambulia makamanda wa  Daesh nchini Syria

Vyanzo vya kijeshi vimeeleza kufanyika shambulio katika kikao cha makanda wa kikundi cha Daesh nchini Syria, shambulio liliofanywa na ndege za kijeshi la Iraq ndani ya Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: ndege za Iraq zashambulia mkutano wa makanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria na kupelekea kuangamia kwa magaidi zaidi 45 nchini humo.
Kamanda wa mashambulizi shirikishi katika majeshi ya Iraq amesisitiza kuwa shambulio liliofanywa na ndege za nchi hiyo katika eneo la ardhi ya Syria, magaidi 54 kuangamia wakiwemo makanda wakuu wa kikundi hicho.
Kwa mujibu wa maelezo ya majeshi ya Iraq ni kwamba, mashambulio matatu yalifanywa katika kambi za kikundi cha kigaidi cha Daesh, kambi ambazo zilichimbwa kwa mahandaki zikiunganisha kambi na kambi zingine mashariki mwaka Syria.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky