Ndege za kivita za Marekani zafanya mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen

 Ndege za kivita za Marekani zafanya mashambulizi  dhidi ya wananchi wa Yemen

Ndege za kivita za Marekani zimefanya mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen na kudai kuwa ilikuwa ikiwalenga wapiganaji wa kundi la kigaidi la al- Qaida nchini Yemeni.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Ndege za kivita za Marekani zimefanya mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen na kudai kuwa ilikuwa ikiwalenga wapiganaji wa  kundi la kigaidi  la al- Qaida nchini Yemeni.

Hakukuwa na taarifa za awali kuhusiana na majeruhi nchini humo. Lakini mashuhuda waliongea na waandishi wa habari kuwa ndege za kivita za Marekani pamoja na ndege zisizokuwa na rubani zilifanya mashambulizi kuilenga wilaya ya al- Sawmaa katika jimbo la Bayda mapema leo asubuhi. Mashambulzi hayo ya anga yamefanyika ikiwa ni mwezi mmoja baada ya vikosi maalumu vya Marekani kuliushambulia jimbo hilo ambapo afisa mmoja wa jeshi la Marekani ambaye alikuwa akiyasaidia majeshi ya Saudia arabia katika kushambulia wananchi wa aliuwawa.

Saudia arabia ikishirikiana na matarifa Zaidi ya 10 ikiwemo Marekani wameizingira Yemen na kushambulia wananchi wa Yemen kwa lengo la kumrudisha madarakani rais Hadi ambaye wananchi wake hawamtaki.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky