Ndugu wa kiongozi wa Korea kaskazini auwawa

Ndugu wa kiongozi wa Korea kaskazini auwawa

Mdogo wake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un ameuwawa nchini Malaysia

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mdogo wake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un ameuwawa nchini Malaysia Shirika la habari la Yonhap na vyombo vya habari nchini Korea kusini vimeripoti leo, vikinukuu duru ambazo hazikutambuliwa. Shirika la habari la Yonhap , limenukuu duru kutoka serikali ya Korea kusini zikisema Kim Jong Nam aliuwawa jana Jumatatu asubuhi nchini Malaysia, lakini hakukutolewa taarifa zaidi. Kituo cha matangazo ya Televisheni cha Chosun, kimesema kwamba Kim alipewa sumu katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur na wanawake wawili wanaoaminika kuwa ni watumishi wa korea kaskazini, ambao walikimbia. Polisi ya Malaysia imelieleza Shirika la habari la Reuters kwamba mtu mmoja kutoka Korea kaskazini ambaye hakutambuliwa alifariki akiwa njiani kwenda hospitali kutoka uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky