Netanyahu: Daesh waondoka Iran yafika

Netanyahu: Daesh waondoka Iran yafika

Waziri mkuu wa serikali ya kivamizi ya Israel amesisitiza kuwa: sisi tunapinga vikali kuwepo kwa Iran na washirika wake mfano wa Hizbullah nchini Syria, hivyo njia yeyote tutafanya ili kukabiliana na suala hilo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Binjamin Netanyahu ambaye ni waziri mkuu wa Utawala haramu wa Israel alisema setesi hii kuwa: kikundi cha kigaidi cha Daesh kimeondoka, Iran yawasili katika sehemu hiyo, huku akisisitiza kuwa kamwe hatutakubali kuiacha Iran na washirika wake, kuyamiliki maeneo yalioachwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Aidha aliashiria kauli ya kiongozi mkuu wa shirika la kijasusi mcjimi Israel {Mossad) kuhusu chamngamoto walizokuwa nazo kuhusu suala la ulinzi na usalama, ambapo changamoto hiyo zinaweza kufupishwa katika sentezi hii kwamba: magaidi wa Daesh waondoka, Iran yaingia. Kwa maana jambo muhimu tunalolizungumzia ni kuhusu hatima ya Syria.
Kiongozi wa Mossad siku ya Jumatatu alielezea hofu yao ya kutanuka wigo wa Iran na washirika wake katika ukanda wa mashariki ya kati kupitia majeshi yake nchini Syria, Yemen, Lebanon na Iraq.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema: mtazamo wetu uko wazi, kwamba tunapinga kuwepo na kuimarika majeshi ya Iran na washirika wake mfano wa Hizbullah nchini Syria, hivyo basi tutatumia njia yeyote ya kukabiliana jambo hilo, hivyo tutaimarisha majeshi yetu ya ulinzi na usalama na kulinda mipaka ya nchi yetu aliyasema hayo Netanyahu.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky