Netanyahu: Iran inalengo la kushambulia Israel

Netanyahu: Iran inalengo la kushambulia Israel

Waziri mkuu wa Israel amedai kuwa lengo la kubaki kwa majeshi ya Iran nchini Syria ni kutaka kushambulia Israel

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri mkuu wa Isreal ambaye kwa sasa yuko nchini Ujerumani, akiendelea na ratiba yake ya kuizulia serikali ya Iran, amedai kuwa Jamhuri ya kiislamu ya Iran inataka kushambuia Israel.
Benjamin Netanyahu ameyasema hayo siku ya Jumatatu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuonana kwake na “Angera Merkel” kiongozi mkuu wa Ujerumani, na kusisitiza kuwa lengo la Iran kufanya juhudi za kubaki kwake nchini Syria ni kutaka kufanya mashambulizi nchini Israel.
Waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel, ambapo utawala wake unavichwa kadhaa vya mabomu ya Nyuklia, amesema kuwa changa moto kubwa iliokuwa nayo ulimwengu wa sasa wa utandawazi ni serikali na majeshi ya Kiislamu ambayo yanafanya juhudi za kumiliki silaha za Nyuklia.
Aidha amesisitiza katika mazungumzo yake hayo kuwa, Iran ni hatari na tisho ulimwenguni hata hivyo  inapwa iondoke haraka nchini Syria, kwani lengo la kubaki Iran nchini Syria ni kurahisisha kufanya mashambulio yake katika utawala haramu wa Israel, jambo ambalo halikubaliki na utawala wa Israel.
Akiendelea kusema kumuambia kiongozi wa Ujerumani kuwa: kama serikali ya ujerumani haitakaza mkanda katika kukabiliana na Iran na ikaacha kutoka katika makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran, Ujerumani itaendelea kuona wakimbizi wengi wa Syria wakizidi kumiminika nchini humo.
Naye kiongozi wa Ujerumani alionga mkonu maneno ya Netanyahu kunako harakati za Iran katika ukanda wa mashariki ya kati na kuisifu kuwa ni changamoto iliopo, ama amesisitiza kusema kuwa ni kweli tunaafikiana kuwa harakati za Iran ni changamoto kwetu, lakini tunatafautia kunako jinsigani ya kukabiliana na Iran, kwa maana kukabiliana njia ya kukabiliana naye si kutoka katika makubaliano ya Nyuklia, pamoja yakuwa lengo letu sote ni kuifanya Iran isiweze kumiliki silaha za nyuklia.
Mwisho alisisitiza kwa kusema kuwa Ujerumani haitaafiki kutoka katika makumbaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran, na tutashirikiana na umoja wa Ulaya katika kushikamana na makubalianao baina ya Ulaya na Iran.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky