Netanyahu: tatizo letu la msingi lipo na Iran si Bashar Asad

Netanyahu: tatizo letu la msingi lipo na Iran si Bashar Asad

Waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel amefanya ziara yake nchini Urusi ambapo katika safari hiyo amaesema: Israel inamatatizo na uadui na Iran na wala si Rais wa Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na “Benjamen Nitanyahu” waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel alipokuwa amefanya ziara yake nchi Urusi, ambapo katika safari hiyo alisema alipojumuika na waandishi wa habari na kusisitiza uadui wa utawala huo haramu na serikali ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine tena.
Baadhi ya magazeti yameandika kuwa: amesema Netanyahu kuwa tatizo lao la asili na msingi lipo na Iran na wala si utawala wa Syria, huku akisisitiza kuwa juhudi kubwa inayofanywa na utawala wa Israel ni kuyatoa makombora ya masafa marefu ya Iran yaliopo nchini Syria na kuzorotesha fungamano la Iran na Syria.
Aidha alisistiza kwamba ni zaidi ya miaka 40 utawala haramu wa Israel haukuwa na tatizo na Basshar Asad, ambapo katika kipindi hicho chote Golan haikuwahi kupigwa hata risasi moja kutoka kwa Syria, jambo lilioanza kutuletea matatizo katika sehemu hiyo ni kuwepo kwa magaidi wa Daesh karibu na mipaka yetu na baada ya hapo kuingia kwa Iran na Hizbullah katika sehemu hizo.
Waziri mkuu wa Israel amesisitiza kuwa: hatuwezi kuvumilia kuwepo kwa Iran karibu ya mipaka yetu jambo linasababishwa na utawala wa Syria ambaye umetoa ruhusa kwa Iran kuwepo katika maeneo hayo.  


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky