Papa Francis asisitiza kuto husishwa uislamu na ugaidi

Papa Francis asisitiza kuto husishwa uislamu na ugaidi

Kiongozi wa kikristo wa dhehebu la Katoliki duniani ambapo amezungumza hayo katika kongamano la kimataifa la taasisi za kijamii duniani asisitiza kuto husika uislamu na vikundi vya kigaidi

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Papa francis aliyasema hayo katika kikao cha kongamano la kimataifa la taasisi za kijamii duniani na kuashiria kuwa ugaidi hauna fungamano na Uislamu
Kiongozi wa Wakristo wa dhehebu la katoliki duniani katika hutuba yake hiyo amebainisha kuwa: kazi ya dini ni kusambaza suluhu, upendo na amani kwa watu, ama suala la vikundi vya kigaidi vipatikana katika dini zote ulimwenguni.
Aidha ameongeza kusema kuwa watu masikini na mafakiri daima wamekuwa wakisngiziwa mambo wasiokuwa wanayafanya kutokana na uchache wa kipato chao, ambapo hutuhumiwa kuwa ni makatili na kuwa wanaroho ngumu, ambapo hufanywa kampeni hiyo kwajili ya kuandaa mazingira ya kuendelea kuyadhulumu mataifa hayo na kuanzisha fita kubwa kwa madai ya kupambana na ugaidi (hali yakuwa wao ndio wamepanga vita hiyo kwaajili kupata masilahi ytao dhidi ya wanyonge).
Amemalizia kwa kusema kuwa: daima katika kila kundi chama na wafuasi wa kila dini kulionekana watu waovu walikuwa na roho ngumu, lakini ukweli ni kwamba ukatili, unyama na ugaidi, hauna msigi wowote katika dini ya Kikristo na Uyahudi na hauna fungamano lolote na dini ya Uislamu.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky