Polisi nchini Tunis auwawa baada ya kushambuliwa na Gaidi nchini humo

Polisi nchini Tunis auwawa baada ya kushambuliwa na Gaidi nchini humo

Jeshi la Polisi nchini Tunisia limetangaza kuwa mmoja kati ya mapolisi wawili waliojeruhiwa jana mkabala na Bunge la nchi hiyo amefariki kufuatia majaraha makubwa alioyapata katika shambulio hilo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Jeshi la Polisi nchini Tunisia limetangaza kuwa mmoja kati ya mapolisi wawili waliojeruhiwa jana mkabala na Bunge la nchi hiyo amefariki kufuatia majaraha makubwa alioyapata katika shambulio hilo.
Kwa mujibu wa ripoti iliotufikia ni kwamba polisi wawili wa jeshi la Polisi la Tunisia jana walishambuliwa na magaidi kwa kutumia kisu, ambapo gaidi mmoja aliwapiga visu askari hao mkabala na bunge la nchi hiyo nchini humo.
Gaidi huyo alikamatwa na majeshi ya nchi hiyo na baada ya kuhojiwa alikiri kuwa anamiaka mitatu sasa amejiunga na vikundi vyenye fikira ya kigaidi na majeshi ya uslama ya nchi hiyo anaamini kuwa ni Mataghuti ambapo kuwauwa wana usalama hao ni jihadi.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky