Polisi wanne wauwawa katika shambulio la Daesh nchini Misri

Polisi wanne wauwawa katika shambulio la Daesh nchini Misri

Polisi wannae wa jeshi la Polisi la Misri wamepoteza maisha baada ya kikundi cha kigaidi cha Daesh kushambulia gari moja katika barabara ya mji wa Alarish kaskazini mwa jangwa la Sinaa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: taarifa za kuuwawa kwa idadi kadhaa ya wanajeshi wa jeshi la Polisi la Misri zimetangazwa nchini humo.

Polisi wanne wa Misri wameuwawa siku ya Jumatano baada ya kushambuliwa gari moja liliokuwa katika barabara ya mji wa Alarish iliopo kaskazini mwa jangwa la Sinaa.

Magaidi waliokuwa na silaha walishambulia gari la moja la Polisi ya nchi hiyo nalupelekea kuuwawa Polisi wanne waliokuwa na vyeo nchini humo.

Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Misri siku ya Jumanne walifanikiwa kuyaangamiza magaidi watatu ambao walikuwa na silaha katika mkoa wa Qanaa uliopo kusini mwa Misri, ambapo mashambulizi hayo yalikuwa na lengo la kusambaratisha kambi moja ya mafunzo ya magaidi hao katika sehemu za milima nchini humo.

Majeshi ya serikali ya Misri daima yamekuwa yanakabiliana na vikundi vya kigaidi vya Daesh katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo hasa sehemu ya jangwa la Sinaa.

Idadi kadhaa ya magaidi hivi karibuni nchini Misri walijiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika jangwa la Sinaa, ndipo wakaanza kufanya mashambuliazi ya kigaidi chini ya bendera ya kikundi cha hicho cha Daesh na kusababisha vifo vya watu wengi wasiokuwa na hatia

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky