Potin: wadhifa wetu kuulinda mpango wa Nyuklia

Potin: wadhifa wetu kuulinda mpango wa Nyuklia

Rais wa jamhuri ya Urusi amesema kuwa baada ya Marekani kutoka katika makubaliano ya Nyuklia wadhifa wetu sisi tuliobaki kuyalinda makubaliano hayo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Vladimir Putin “rais wa jamhuri ya Urusi” alisema akiwa na mabalozi wa Urusi katika mataifa mengine amesema: baada ya Marekani kutoka katika makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran, wadhifa wetu tunapaswa tutafute njia ambayo itazuia machafuko na kuto elewana katiaka suala hilo.
Aidha ameongeza kusema kuwa makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran ni makubaliano muhimu ambayo yatazuia kuenea kwa uzalishaji wa silaha za Nyuklia Duniani, hivyo basi wadhifa wetu kwa sasa ni kuyalinda makubaliano hayo na kuto ruhusu kuendelea kwa marumbano katika ukanda wa mashariki ya kati.
Putin kwa upande mwingine wa maelezo yake ameonyesha matumaini ya kutatua mgogoro wa masuala ya silaha za nyuklia wa Korea ya kaskazini na kufikiwa tija nzuri.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky