Putin aamuru majeshi yake kuondoka nchini Syria

Putin aamuru majeshi yake kuondoka nchini Syria

Vladimir Putin asubuhi ya leo ametoa amri ya kwamba majeshi yanapaswa kuondoka katika ardhi ya Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa leo na Rais wa Urusi Vladimir Putin kwamba majeshi ya Urusi yanapaswa kuondoka nchini Syria, ambapo alitoa amri hiyo alipokuwa katika kambi ya jeshi la anga ya Samimi nchini humo.
Kambi ya majeshi ya anga ya Samimi, ni kambi ambayo majeshi ya Urusi yalikuwa yameifanya sehemu hiyo kuwa ndio makazi ya majeshi hayo nchini Syria, Rais wa Syria alimpokea Rais wa Urusi katika kambi hiyo akiwa na kamanda wa majeshi ya Urusi.
Rais wa Urusi alisema alizungumza na wanajeshi wake waliokuwa katika kambi hiyo na kumtaka mkuu wa majeshi hayo kufanya maandalizi ya kuondoka nchini humo na kuyaacha majeshi ya Syria kuendeleza kumalizia sehemu iliobaki ya kuwasambaratisha magaidi nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky