Putin: hali ya dunia kwa sasa inatia huzuni

 Putin: hali ya dunia kwa sasa inatia huzuni

Rais wa jamhuri ya Urusi ametangaza kuwa uhalisia wa ulimwengu kwa sasa unatia hofu na huzuni, ama kwa upande wetu tuna matumaini ya kuifanya hali itengamae na kutulia, hatimaye nidhamu sahihi inayoendana na ubinadamu na akaili kutawala dunia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na (Vladimir Putin) Rais wa jamhuri ya Urusi ambapo amebainisha kuwa ulimwengu kwa sasa unaelekea pabaya ambapo hali inasikitisha sana na mambo kutokuwa sawa, ama nina matumaini ulimwengu utarudi katika utarudi katika nidhamu yake na akili itashika nafasi yake na kuhukumu dunia.
Aidha Putin amesema kuwa: Urusi daima imekuwa ikiendeleza siasa za kudumisha na kustawisha usalama na amani Duniani nzima na uakanda wa mashariki ya kati, alkadhalika kwa upande mwengine Urusi itaendelea kushikamana na ahadi na kanuni za kimataifa.
Mwisho amemaliza kwa kuashiria kuwa hali ya Dunia hairidhishi ambapo siku hadi siku dunia inaelekea katika marumbano na mivutano, huku akibainisha kuwa, pamoja na hayo yote bado nina matumaini kuwa nukta ya ushirikiano na umoja wa kibinadamu itashika hatamu na mafungamano ya kimataifa itafikia katika muhula wa ustawi wa jamii na kufanya mambo kwa mujibu wa matashi ya akili, ambapo itapelekea kutengamaa na kukaa sawa mfumo wa kuindesha Dunia.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky