Qatar yatoa vithibitisho kuwa Saudia na Emirates zinasaidia kikundi cha kigaidi cha Daesh na Akaida

Qatar yatoa vithibitisho kuwa Saudia na Emirates zinasaidia kikundi cha kigaidi cha Daesh na Akaida

Serikali ya Qatar imetoa vielelezo vinavyo thibitisha kuwa serikali ya Saudi Arabia na Emirates hutoa misaada kwa viongozi wa vikundi vya kigaidi vya Akaida na Daesh nchini Yemen

Shirikia la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: televishen ya Almayadini katika ripoti zake zimetangaza kuwa: Qatar yafichua vielelezo ambavyo vinaonesha kuwa serikali ya Saudi Arabia na Emirates hutoa misaada kuvisaidia vikundi vya kigaidi vya Daesh na Alkaida nchini Yemen.
Aidha televishen ya Almayadini siku ya Jumatano emetoa ripoti yakwamba kuna vielelezo vya kidiplomasia kutoka ubalozi wa Qatar mjini Washington Marekani, kuwa mwezi Oktoba uliopita ambapo balozi huyo alikabizi vielelezo hivyo kwa Muhammad bin Abdurahman (waziri wa mambo ya nje wa Qatar) ambavyo vinaonesha kuwa Muhammad bin Salmani (ambaye anatarajiwa kushika ufalme wa Saudia baada ya kufa baba yake) na Muhammad bin Zaid (anaetarajiwa kuwa mfalme wa Emirates) wametoa misaada kwa magaidi wa Daesh na kikundi cha Alkaida viliopo nchini Yemen.
Kwa mujibu wa vielelezo hivyo: naibu waziri wafedha nchini Marekani amesema kuhusu masuala ya kigaidi kuwa: mtoto wa mfalme wa Saudia na mtoto wa mfalme wa Emirates walionana na Ali Abkaru Hasan na Abdallah Faisal Al-Ahdal ambaye ni myemen, ambapo wote wawili ni katika magaidi ambao wanafungamano kubwa na kikundi cha kigaidi cha Alkaida.
Aidha katika vielelezo hivyo imeelezwa kwa wazi kabisa kuhusika kuwa watu hao wawili mafungamano makubwa na viongozi wakubwa wa kikundi cha kigaidi cha Alkaida, kwa upande mwingine misaada ya kipesa imeonekana ikitolewa moja kwa moja kutoka kwa Khalid bin Ali bin Abdallah Alhamidani (ambaye ni taasisi ya usalama na ulinzi ya Saudi Arabia) na kupewa Ali Abkar kwaajili ya kununua vifaa vya kijeshi na kuviwasilisha kwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Naibu waziri wa pesa nchini Marekani amethibitisha kuwa ibn Salman, ambaye ndiye anatarajiwa kuwa mfalme wa Saudi Arabia baada ya kufa baba yake, ameonekana kuwa na mawasiliano na kikundi cha kigaidi cha Akaida pamoja na vikundi vingine vya kigaidi bila ya kuunganishwa na serikali ya Washington, kitu ambacho kinaleta mashaka, alisema naibu waziri huyo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky