Rais amenitaka nisubiri kidogo kuhusu ombi la kujiuzulu kwangu

Rais amenitaka nisubiri kidogo kuhusu ombi la kujiuzulu kwangu

Waziri mkuu wa Lebanon amesema alipokuwa katika ikulu ya Lebanon kuwa; leo nimekabidhi ombi langu la kujiuzulu kwangu kwa Rais wa Jamhuri ya Lebanon (Michel Aoun)

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Saad Hariri waziri mkuu wa Lebanon aliyasema hayo katika ikulu ya jamhuri ya Lebanon huku akiashiria kuwa ombi lake la kutaka kujiuzulu ameliwasilisha kwa Rais wa nchi hiyo Michel Aoun
Aidha ameongeza kusema kuwa: Michel Aoun ameniomba nisubiri kidogo ili fanye uchunguzi wa kina kuhusu suala la kujiuzulu kwake, nami pia nimekubali umbi lake.
Waziri wa mambo ya nje wa Lebanon amebainisha kuwa Lebanon inahitaji juhudi ya pande zote zishirikiane katika kuliepusha taifa hilo hatari mbali mbali.
Saad Hariri amebainisha kuwa matumaini yake ni ushirikiano wa dhati na pandie zote husika kwaajili ya kusaidia kuijenga Lebanon.
Waziri mkuu wa Lebanon amerudi nchini kwake asubuhi ya siku ya Jumatano akitokea nchini Saudi Arabia, ili kuthibitisha tangazo la kujiuzulu kwake alilotangaza mjini Riyadh mji wa Saudi Arabia.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky