Rais wa Azarbaijan amteuwa mke wake kuwa ni naibu wake wa kwanza

Rais wa Azarbaijan amteuwa mke wake kuwa ni naibu wake wa kwanza

Rais wa jamhuri ya Azerbaijan leo siku ya Jumanne amemuanisha mke wake kuwa naibu wake wa kwanza katika serikali ya nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Rais wa jamhuri ya Azarbaijan amefanya uteuzi huo leo siku ya Jumanne, ambapo amemteuwa mke wake aliyekuwa na umri wa miaka 52 kuwa naibu wake wa kwanza.
Mke wa Rais huyo (Mehriban Aliyeva) muda mrefu alikuwa akijishughulisha na masuala ya kisheria, huku akiwa msimamizi wa taasisi za kifadhili na misaada nchini humo.
Mnamo mwaka 2003 Ilhamu Aliyev (Rais wa nchi hiyo) alirithi cheo hicho baada ya kufa baba yake (Heydar Aliyev) na kuwa rais wa Jamhuri ya Azerbaijan.
Heydar Aliyev awali alikuwa kiongozi wa chama cha Kikomonisti nchini humo katika kipindi cha serikali ya Urusi ya zamani, na baada ya kuanguka utawala wa Urusi ya zamani akawa Rais wa jamhuri ya Azerbaijan.
Ilham Aliyev aliokuwa na umri wa miaka 55 alikuwa katika wanao jiegemeza upande wa serikali za Ulaya, ama uhusiano huo umeingia dosari baada ya mataifa ya kimagaharibi kuikosoa serikali yake inapingana na haki za binadamu baada ya kutokana na kupambana na vikundi vinavyo mpinga nchini humo.
Kwa mujibu wa mitazamo wa vyama vinampinga Aliyev kwamba: suala la katiba ya nchi hiyo na kuongeza muda wa Urais katika katiba ya nchi hiyo, ndio sababu ya nchi hiyo kuelekea upande wa kifalme    
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky