Rais wa Urusi ayataka majeshi yake ya anga kufanya maandalizi ya vita

Rais wa Urusi ayataka majeshi yake ya anga kufanya maandalizi ya vita

Waziri wa ulinzi wa Urusi amesema: Vladimir Putin ametoa amri ya kufanya maandalizi na kuweka mambo vizuri kwa majeshi ya nchi hiyo kwaajili ya kufanya shambulio zito la ghafla

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Vladimir Putin “Rais wa Jamhuri ya Urusi” ameliamuru jeshi la anga la nchi hiyo kujiandaa kwaajili ya kuanza vita.
Hayo yamesemwa na waziri wa ulinzi wa Urusi: kwamba Rais wa nchi hiyo ameamuru kufanywa uchunguzi na ugaguzi katika majeshi ya nchi hiyo ili kundaa kutoa pigo kubwa la kijeshi la ghafla.
Aidha Rais wa jamhuri ya Urusi ameamuru kufanya utafiti ili kufahamu hali iliopo ya majeshi na taasisi za kijeshi na majeshi ya nchi hiyo kuhusu maandali ya vita nchini humo.
Alkadhalika jeshi la nchi hiyo ametaka kufanya hivyo ili kujua sistimu ya kivita nchini humo, kiasi gani ipo na utayari wa kimashambulizi ya kiviita.
Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo amesema kuwa: kwa mujibu wa amri hiyo, makamanda wakuu wa jeshi la nchi hiyo, wameanza uchunguzi huo katika kufahamu maandalizi ya jeshi la anga la kufanya shambulio zito la ghafla, pia kujua utayari wa wanajeshi wa majeshi hayo na vitengo vyake husika katika kutekeleza nyadhifa zao katika viwanja vya mapambano.
Amri ya rais wa Urusi imetokea katika hali ambayo hofu za kuingezeka kwa mvutano bainaya serikali ya Urusi na nchi za Ulaya, ambapo kwa upande mwingine kumekuwepo na mahusiano mabaya baina ya Urusi na nchi za NATO
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky