Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh auawa

Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh auawa

Wizara ya ndani ya Yemen imetangaza kuuawa kwa Ali Abdullah Saleh kupitia kituo rasmi cha televisheni cha Al-Masirah

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Wizara ya ndani ya Yemen imetangaza kuuawa kwa Ali Abdullah Saleh kupitia kituo rasmi cha televisheni cha Al-Masirah

Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh ameuawa. Taarifa hiyo imethibitishwa na wizara ya ndani  inayodhibitiwa na wapiganaji wa  kihouthi nchini Yemen baada ya kuibuka video iliyoonekana ikiionesha maiti ya Abdullah Saleh. Haya yanajiri huku kukiwa na mapigano makali katika mji wa Sanaa kufuatia fitana nzito ya rais huyo.

Chama cha rais huyo wa zamani GPC kimethibitisha kuuawa kwake. Kiongozi wa chama hicho Faiqa al-Sayyid amewalaumu wapiganaji wa  kihouthi kwa kumuua Saleh. Faiqa ameeleza kuwa Saleh pamoja na wakuu wengine wa chama waliuawa walipokuwa wakikimbia mji wa Sanaa unaodhibitiwa na wapiganaji wa  kihouthi wakielekea maeneo ambayo yanadhibitiwa na vikosi vitiifu kwake.

Kwa mujibu wa duru ya kijeshi, watu wasiojulikana walisimamisha msafara wa magari 4 ya Saleh takriban kilomita 40 kusini mwa Sanaa, wakampiga risasi Saleh na kumuua. Aidha walimuua Katibu Mkuu wa chama Arif al-Zouka na naibu wake Yasir al-Awadi.

Wizara ya ndani ya Yemen imetangaza kupitia kituo rasmi cha televisheni cha Al-Masirah kwamba mzozo wa wanamgambo umemalizika kufuatia kuuawa kwa Saleh ambaye alikuwa kiongozi wao pamoja na wafuasi wake kadhaa waliokuwa na silaha.

Tangazo la kuuawa kwa Abdullah Saleh limejiri baada ya video iliyoonesha kile kilichoaminika kuwa maiti ya Saleh iliyofunikwa kwenye blanketi huku kichwa kikiwa na jeraha baya, kuanza kusambaa katika mitandao ya kijamii. Video hiyo haijathibitishwa

Kusambaratika kwa muungano wa waasi

Akitangaza taarifa hiyo, mtangazaji wa televisheni ya Al-Masirah amesoma: "Wizara ya ndani inatangaza mwisho wa wapiganaji wa  kihouthi kwa kuchukua udhibiti wa maeneo yao na kurejesha usalama katika mji wa Sanaa, viunga vyake na katika mikoa yote. Pia inatangaza kuuawa kwa kiongozi wa wasaliti na baadhi ya wapambe wake."

Mapema leo, wapiganaji wa  kihouthi wa Kishia wanatuhumiwa kuripua nyumba ya Saleh mjini Sanaa, muda mfupi baada ya kuivamia. Wahouthi pia walidai kuchukua udhibiti wa maeneo kadhaa ambayo vikosi vitiifu kwa Saleh vilikuwa vikidhibiti na kuongeza kuwa mamia kadhaa ya wanamgambo hao walijisalimisha.

Kulingana na Kamati kuu ya shirika la Msalaba Mwekundu , watu 125 wameuawa na 238 wamejeruhiwa katika mapigano hayo ya hivi karibuni.

Saleh alitawala Yemen kwa miongo mitatu na kufanya ufisadi mkubwa

Mnamo Jumamosi, Saleh alitangaza mwisho wa ushirikiano wake na wapiganaji wa  kihouthi na kuunga mkono Saudia arabia inayoshambulia wananchi wa Yemen.

Saleh aliyekuwa na umri wa miaka 75, na mwenye nguvu alitawala Yemen kwa zaidi ya miongo mitatu hadi alipoondolewa kufuatia shinikizo la kisiasa mwaka 2012 huku akiwa amejilimbikizia utajiri wa hali ya juu.

Lakini alisalia nchini humo na kuendelea kuwa na ushawishi wa mamlaka kwa mlango wa nyuma. Licha kwamba aliwahi kupambana na wanamgambo wa Wahouthi mara kadhaa, mnamo 2014 vikosi vyake vilishirikiana na Wahouthi. Muungano huo uligawika  wiki iliyopita na kusababisha mapigano makali kati ya Wahouthi na vikosi vya Saleh.

Mapigano kati ya pande hizo mbili yalianza Jumatano wiki, Pande zote mbili zimekuwa zikilaumiana kufuatia vita hivyo.

Ndege za kivita za muungano unaoongozwa na Saudi Arabia zimekuwa zikifanya mashambulizi katika wapiganaji wa  kihouthi na maeneo ya makazi ya wananchi nchini Yemen na kuua mamia ya watu wasio na hatia.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky