Rais wa zamani wa Yemen, asema yuko tayari kufanya mabadiliko

Rais wa zamani wa Yemen, asema yuko tayari kufanya mabadiliko

Saudia arabia ambayo inadai kuwa mwakilishi wa uislamu inafanya unyama wa hali ya juu dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdallah Saleh amesema yuko tayari kufanya mabadiliko na kurejesha mahusiano pamoja na muungano wa majeshi ya nchi 11 unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya wananchi wa Yemen vinavyoendelea kwa muda wa miaka mitatu sasa.

Kauli hiyo ya Ali Abdallah Saleh kwamba anataka sasa kuzungumza na utawala wa Saudi Arabia ameitoa wakati ambapo uhusiano wake na kundi la wapiganaji wa Huthi linalotetea haki za wayemen unalegalega.  Wakati hayo yakiendelea wapiganaji wanaomuunga mkono kiongozi huyo wa zamani wa Yemen wanaendelea kupambana na wapiganaji wa kundi la Houthi kwa siku ya tano katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Televisheni ya Al Arabiya inayomilikiwa na Saudi Arabia imeripoti kuwa takriban watu 80 wameuawa katika mapigano hayo kati ya wapiganaji waaminifu kwa Saleh na kundi la wapiganaji wa Huthi. Migogoro kati ya pande hizo mbili zilizokuwa zamani washirika imeongezeka katika miezi ya hivi karibuni, huku wafuasi wa Saleh wakiwalaumu kundi la wapiganaji wa Huthi kwa kujaribu kujiongezea madaraka na wa huthi wakiwalaumu wenzao kwa kuwa na sura mbili.

Katika hotuba yake kwenye televisheni Saleh ametoa wito kwa ndugu zake katika nchi jirani wa  kuacha vitendo vya uchokozi na badala yake amewaomba waondoe vizuizi dhidi ya Yemen na wao wako tayari kuufungua ukurasa mpya.Saleh pia ameahidi kwamba, baada ya mapigano kusitishwa na vizuizi kuondolewa watakuwa tayari kushiriki katika majadiliano ya moja kwa moja kupitia mamlaka halali inayosimamiwa na bunge la Yemen. Maoni yake yamepokewa kwa furaha na muungano wa majeshi unao ongozwa na Saudi Arabia kwani muungano huo umeshashindwa kufikia malengo yake kwa kutumia vita. Wahusika katika muungano huo wameeleza kuwa wanayaamini na kuyaunga mkono mapendekezo ya viongozi na wahusika wa chama cha Ali Abdalla Saleh cha General People's Congress (GPC). Saleh na wafuasi wake wanataka kurudisha ushirikiano na nchi za Kiarabu.

Saudi Arabia imekuwa inauongoza ushirikiano wa mataifa ya Kiarabu yanayofuata madhehebu ya Sunni na wamekuwa wakipigana na wananchi ya Yemen ambao asilimia kubwa ni Mashia tangu mwanzoni mwa mwaka 2015. Nchi za Kiarabu hivi karibuni ziliweka vizuizi vya kijeshi kote nchini Yemen baada ya kundi la wapiganaji wa Huthi wa nchi hiyo kurusha kombora lililofika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh na kusababisha hasara kubwa licha ya kuwepo kinga za makombora kutoka Marekani.

Kufika kwa makombora hayo mpaka mji mkuu wa Saudia Arabia, kumeonyesha udhaifu wa kinga za makombora ya Marekani na kuleta sintofahamu.

Yemen ni mojawapo ya nchi zilizo masikini zaidi duniani. Tangu mwaka 2015, inakabiliwa na vita vinavyoendeshwa na Saudia arabia. Saudi Arabia na washirika wake kutoka nchi 11 wanapambana na wananchi wa Yemen ambao wanampinga rais Hadi ambaye ni kibaraka wanchi za magharibi . Nchi hiyo imekumbwa na janga la kibinadamu, watu zaidi ya 10,000 wameuawa na majeshi  ya Saudia arabia huku umoja wa mataifa ukiwa kimya.

Watu wengine karibu milioni 2 wamelazimika kuyahama makazi yao. Pamoja na hayo mkurupuko wa maradhi ya kipindupindu umewaathiri takriban watu milioni 1. Wakati huo huo nchi hiyo pia inakabiliwa na kitisho kikubwa cha njaa.

Saudia arabia ambayo inadai kuwa mwakilishi wa uislamu inafanya unyama wa hali ya juu dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen, huku ikijisifu kwa ukatili huo.

Mwisho wa habari / 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky