Saad Hariri ajiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu wa Lebanon

Saad Hariri ajiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu wa Lebanon

Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimetangaza kujiuzulu kwa waziri mkuu wa Lebanon (Saad Hariri) katika nafasi yake ya uwaziri mkuu

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimesambaza habari ya kujiuzulu kwa Saad Hariri katika nafasi yake uwaziri mkuu nchini Lebanon.
Televishen ya Alhadath katika ripoti zake imetangaza kuwa Saad Hariri, waziri mkuu wa Lebanon ambaye kwa sasa yoko nchini Saudi Arabia amejiuzulu nafasi yake ya uwaziri mkuu nchini humo.
Hariri anakhofu ya kuuliwa nchini Lebanon, huku akibainisha kuwa hali ya sasa nchini Lebanon inashabihiana na hele iliokuwa kabla ya kuuliwa kwa Rafiqi Hariri.
Waziri mkuu wa Lebanon katika maelezo yake ya kustaajabisha amesema: tutaikata mikono ya Iran katika ukanda wa mashariki ya kati.
Aidha ameendelea kusema: kamwe sitakubali Lebanon kuwa ndio sehemu na chanzo cha tushio la amani ya mashariki ya kati; pia sikubali silaha za Hezbullah zitumike katika kuwauwa wananchi wa Syria.
Pia amedai kuwa lengo kubwa la Iran ni kuharibu na kusambaratisha Waarabu, huku akisisitiza kuwa shari alioeleta Iran katika ukanda wa mashariki ya kati, itamrejea yeye mwenyewe.
Kujiuzulu kwa Saad Hariri kumetokea moja kwa moja baada ya safari mbili mfululizo za kwenda Saudi Arabia na kufanya vikao vya mara kwa mara na viongozi wa Saudi Arabia.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky